Timu ya Yanga imekitaja kikosi chake kitakachoanza leo kwenye mechi yake
dhidi ya wenyeji wao Madeama SC ya Ghana kwenye hatua ya makundi ya
kombe la shirikisho.
Julai 16 mwaka huu timu hizo zilikutana kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam walitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.
Timu ya Yanga inatakiwa ishinde kwenye mechi hiyo ili ijiweke kwenye
mazingira mazuri ya kuwania nafasi mbili za kufuzu kwenye kundi lake
ikiwa kwa sasa inaburuza mkia ikiwa na pointi moja na Tp Mazembe ndiyo
wanaongoza kundi hilo wakiwa na point saba.
Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amewataja wachezaji 11
watakaoanza kwenyemechi hiyo akiwemo Deogratius Munish, Juma Abdul,
Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Mbuyu Twite, Saimon Msuva,
Thaban Kamusoko, Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.
Wachezaji wa akiba ni pamoja na Ally Mustafa, Vicent Andrew, Said
Juma, Pato Ngonyani, Juma Mahadhi, Amissi Tambwe na Malimi Busungu. Kila
la kheri kwa timu ya Yanga kwa kuwa wao ndiyo wawakilishi pekee kutoka
Tanzania kwenye mashindano hayo makubwa.
Tuesday, July 26, 2016
Home »
HOME
» Hiki ndicho kikosi cha Yanga kitakachoanza kwenye mechi yake ya leo dhidi ya Madeama SC
0 comments:
Post a Comment